Alhamisi, 26 Septemba 2013




MKUU wa mkoa wa kusini Pemba Juma Kassim Tindwa, akizungumza na wanajumuia ya JUKAMKUM hawapo pichani kabla ya uzinduzi wa mradi maalum wa kuwafikia vijana 80 wanaotumia dawa za kulevya na waliokatika mazingira hatarishi ya kutumia dawa hizo, hafla hiyo ilifanyika uwanja wa Gombani Chake chake Pemba, kulia ni mjumbe wa JUKAMKUM Fatma Marzouk Kombo na kushoto ni Mussa Mohamed (picha na Haji Nassor, Pemba)

Ijumaa, 20 Septemba 2013

'KAZALIWA 1985- KAFA 2013' Aliekuwa mpiga picha wa kujitegemea kutoka 'the best photo studio' ya mjini Chake chake, Ali Khatib Haji, ambae amefariki dunia tarehe 19/09/2013 majira ya saa 2:40 baada ya kijana huyo kuigonga gari, yeye akiwa na vespa wakati gari hiyo ikikatisha kuelekea Tibirinzi karibu na benki ya watu wa Zanzibar PBZ mjini Chake chake, na kijana huyo akitokea mjini kwenda upande wa Machomane. 

'KAZALIWA 1985-2013 KUFA' Aliekuwa mpiga picha wa kujitegemea ''the best photo studio', Ali Khatib Haji wa mji wa Chake chake, akiwa kazini kabla ya kifo chake katika skuli ya Michakaini Chake chake, kijana huyo alifariki kutoka na ajili ya gari baada ya yeye kuigonga gari kwenye eneo la benki ya watu wa Zanzibar PBZ Chake chake, wakati gari ikikaisha kwenda Tibirinzi, tarehe 19/09/2013 saa 2:40 usiku. 

'UWANJA FRESH SOKA JE' Ni uwanja wa Gombani Chake chake Pemba, ambao kwa sasa umeshawekea nyasi bandi, haya ni matunda ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, ambapo kwa sasa yanatimiza miaka 50 kwa mwaka 2014, sasa uwanja upo lakini soka je ? (picha na Haji Nassor, Pemba) 

Alhamisi, 19 Septemba 2013

'ELIMU MUHIMU' Afisa Mkuu wa huduma na elimu kwa walipa kodi kutoka TRA Zanzibar, Saleh Haji Pandu (aliesimama akiwa amevaa tai) akizungumza na wafanyabiashara wa Kisiwa cha Pemba, kwenye ukumbi wa hoteli ya HIFADHI ZSSF Pemba hivi karibuni (picha na Haji Nassor, Pemba)

Jumamosi, 7 Septemba 2013

 ''DAR-MPAKA SOUZ'' Mmiliki wa blog hii kushoto mwenye kofia Haji Nassor, akikabaidhiwa TUZO ya uhsindi wa kuwasilisha makala za JINSIA mwezi Machi 2013 huko hoteli ya Blue Parl Ubungo jijini Dar es Salaam, ambapo baadae  mwezi April , 2013 sasa safari ikiwa ni SOUZ kwa ajili ya kuiwalikisha Tanzania katika kazi kama hiyo, ingawa hakufanikiwa kushina namba moja.''NIASHINDA? Mmiliki wa blog hii mwenye kofia akifuatilia kwa karibu matokeo ya uwasilishaji wa makala za jinsia Jijini Dar, ambapo badae alishinda na kukabidhiwa tuzo na GENDER LINK


'SIJUI KUWA WATAAJIRIWA HALAFU' Vijana wa kikosi kazi cha Skaut kisiwani Pemba kikiwa katika onyesho maalum kwenye kilelel cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana ambapo kwa Zanzibar yalifanyika uwanja wa Madungu Chake chake Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)


'ONA BABA' Ni moja katia ya matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo yamejengwa uhai wa rais wa kwanza wa Zanzibar na mkombozi wa taifa hili Abied Amani Karume, ambpo hoteli hii ya SMZ ilioko Wete Pemba, kwa sasa imeachwa na kuchakaa ndio hiyo.


''URAIS UNAANZIA HAPA' Wanafunzi wa skuli ya Maandilizi Gombani Chake chake wakiwa katika matayarisho ya masomo. ambapo hadi mwaka 2013 wanasoma ndani ya msikiti uliopo Gombani (picha na Haji Nassor, Pemba)

Ijumaa, 6 Septemba 2013


 'AMA HILI GOLI' Mshambuliaji wa timu ya Kiziambani aliembele na mpira akiwa ameshampita mlinzi wa timua ya Jamhuri Seif Saleh ambapo mshambuliaji huyo Mfanyeje Mussa alifanikiwa kuipatia timu yake goli la pili, kwenye mchezo wa Ligi kuu ya Zanzibar uliochezwa Septemba 6, 2013  uwanja wa Gombani ambapo Kiziambani ILISHINDA kwa magoli 2-0 (picha na Haji Nassor, Pemba)

'HAMUPITI HAPA' Mwenye jezi no 6 ni mlinzi wa timu ya Kizimbani Ali Othuman Ali, akisaidiana na mlinzi mwenzake mwenye jezi no 17 Mohamed Juma Mohamed wakiwazuia washambuliaji wa timu Jamuri kwenye mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliochezwa Septemba 6, 2013 uwanja wa Gombani, ambapo Kizimbani ILISHINDA kwa magoli 2-0 (picha na Haji Nassor, Pemba) 


 'CHUNGA KICHWA CHAKO TU' Mchezo kiumbizi ambao ulikuwa marufu sana katika kijiji cha Pujini Wilaya ya Chake chake, sasa umeonekana kupotea kwa kasi na kuonekana kwenye sherehe za kitaifa pekee (picha na Haji Nassor, Pemba)

'KWANZA NAKATA UTEPE' Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar balozi, Seif alipofika Chambani Wilaya ya Mkoani, kufungua skuli ya kijiji hicho, akishuhudiwa kwa karibu na Naibu Waziri wa Elimu Zanibar Zahara Ali Hamad (picha na Haji Nassor, Pemba)

''TUMIA AKILI YAKO' Waandishi wa habari kutoka nchia 12 za Asiam Afrika, Ulaya na Amerika ka kusini na kasakazini wakiwe kwenye mafunzo maalum nchini, China juu ya hatua iliofikiwa na China na katika suala zima la uwandishi wa habari

Jumatano, 4 Septemba 2013

'MCHAMA AGO HANYELE'' Wanawake wa Wilaya ya Micheweni Pemba wakiwa kazi zao wa kusuka na kupakasa ukili kwa ajili ya mikoba, makawa ya ukindu ambayo ndio mikoba ya asili tokea miaka ya 40 (picha na Haji Nassor, Pemba)

AENDA JELA MIAKA 60 KWA UBAKAJI WA MAPACHA 
Na Haji Nassor, Pemba
MAHAKAMA ya Mkoa Chake chake, imemuhukumu kifungo cha miaka 60 jela, mshitakiwa Abubakar Mkulu Bakar (28), mkaazi wa Wambaa Mkoani, baada ya kubainika na kosa la kuwabaka watoto wawili mapacha wa kike (13).
Kijana Abuu ametakiwa kutumikia jela kwa muda wa miaka 30 kwa kila mtoto mmoja, baada ya Mahakama hiyo kutosheka na ushahidi uliotolewa na mashahidi sita akiwemo Daktari na watoto wenyewe ambao walibakwa kwa muda wa miaka miwili mfululizo.
Licha ya adhabu hiyo ya kutumikia jela 60, mshtakiwa huyo alitakiwa kulipa fidia ya shilingi laki 200,000 (shilingi laki mbili) kutokana na madhara makubwa aliyowasababishia watoto hao.
Kabla ya mshitakiwa huyo, kupewa adhabu hiyo, upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na mwanasheria wa Serikali Ali Bilali Hassan alisema, kuwa hakuna rikodi ya kosa kama hilo lakini mshtakiwa ana makosa mengine kadhaa Mahakamani hapo.
Bilali alidai kuwa vile vile Mahakama iangalie kosa ambalo mshtakiwa ametiwa nalo hatiani kwamba ni makosa yaliyozoeleka katika jamii hivyo aliomba Mahakama kumpa adhabu kali mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia kama hiyo.
‘’Muheshimiwa Hakimu naiyomba Mahakama yako tukufu kumpa adhabu kali mshtakiwa huyu, ukizingatia jamii inaisema sana Mahakama kutokana na makosa kama haya kwamba hayapatiwi ufumbuzi na kupelekea kuongezeka siku hadi siku ‘’alisema Bilali .
Baada ya hapo, Hakimu Khamis Ramadhan ,alimpa nafasi mshtakiwa, na kuiomba Mahakama imfikirie kwa kumpunguzia adhabu kutokana na kukaa rumande kwa muda mrefu, na kwamba anafamilia inayomtegemea ombi ambalo lilitupwa na Mahkama.
‘’Kama  Mahakama imenitia hatiani, Muheshimiwa Hakimu kutokana na tuhuma hizi zidi yangu, naiyomba inionee huruma kwa kunipunguzia idadi ya miaka, ambayo imeniandikia juu ya kosa hili, ambalo lilipangwa juu yangu’’, alidai Abuu.
Awali mshitakiwa  Abubakar  Mkulu Bakar, alitenda kosa hilo baina ya mwaka 2011 na mwaka 2013 huko Wambaa Mkoani ,Tanga na Mwanza Tanzania baram ambapo ilithibitisha kuwabaka watoto hao kwa pamoja na kuwasababishia maumivu makali katika sehemu zao za siri.
Kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu 125 (1) (2) (e) na kifungu 126 (1) sharia namba 6 ya mwaka 2004, sheria ya Zanzibar iliyopitishwa na baraza la wawakilishi Zanzibar, ambapo pia Mahakama hiyo imetoa haki ya rufaa ndani ya siku 30 kukara rufaa kwa yeyote asieridhika na hukumu hiyo.
Hivi karibuni Mahakama hiyo ya Mkoa Chake chake, ilimuhukumu kifungo cha miaka 15 jela, mshitakiwa Issa Ali Mohamed (28), baada ya kutiwa hatiani kwa  kosa la kubaka mtoto wa kike (5) na Ali Mohamed Ali (22) mkaazi wa Kwale Miburani, kifungo cha miaka (30) jela, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike (12).


………………………………………………….. MWISHO ……………………………………………………….