Ijumaa, 30 Agosti 2013


'RAHA YA HABARI ZA VIJIJINI' MWENYE kofia mbele ni Katibu wa 'Jambo group' Hafidh Juma Ali akiwa amefuatana na waandishi wa habari, wa pili Omar Hassan kutoka chuo cha habari TSJ, mara baada ya kumaliza mahojiano na wanajambo Group juu ya maendeleo ya ushirika wao (picha na Haji Nassoor, Pemba)

'RURAL REPORTING' Waandishi wa habari waliowengi wamekuwa wakibakia mjini kwa ajili ya kuandika habari za semina, makongamano na kuwaandikia wanasiasa pekee, mmiliki wa blog hii (HAJI NASSOR) kushoto akizungumza na Mjumbe wa Jambo Group iliopo kwanzani Wambaa Mkoani Pemba Mkubwa Haji Bakar, wakati timu ya waandishi wa habari wa Gazeti la Zanzibar leo walipofika kijijini huko (picha na Omar Hassan TSJ)


'UTAJIRI HUU' Uanikaji wa zao la karafuu kwenye majamvi ndio haswa unaoshuriwa na ZSTC, wakieleza kuwa kufanya hivyo ni kudhibiti ubora na kiwango cha karafuu zenyewe na kinyume chake ni kupoteza ubora wake, (picha na Haji Nassor, Pemba)

'WAKO WAPI WAKANDARASI? Jengo la Wizara ya fedha Pemba ambalo liliporomoka kabla ya ujenzi wake kumalizika, na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi kwa SMZ, sasa jiulize mkandarasi wa Jengo hili yuko wapi (picha na Haji Nassor, Pemba)

''KULIMA PEKE YAKO KUVUNA........

 

 

''SOGEA HUKO'' WANANCHI wa shehia ya Matele Chambani Mkoani Pemba, wakijumuika pamoja katika ujenzi wa barabara yao kwa kiwango cha kifusi, ujenzi unaofadhiliwa na TASAF awamu ya Pili, (picha na Haji Nassor, Pemba)

Jumatano, 28 Agosti 2013


WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo Mgogoni Pemba, akizunguma katika kongamano la vijana, la bara la katiba lililoandaliwa na Jumuia ya Vijana Kaskazini Pemba (NPYO) , kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Said Massoud na kushoto na Mhadhiri wa Chuo kikuu Zanzibar SUZA, Ali Haji Vuia (picha na Haji Nassor, Pemba)

Jumamosi, 24 Agosti 2013

MENEJA wa Islamic benki tawi la Chake chake Pemba Yussuf Ali akizungumza na watendaji wa SMZ Pemba ambapo aliwataka kuwahimiza wafanyakazi wao kuchukua mikopo kwenye tawi hilo, picha na Haji Nassor, Pemba

MMILIKI wa blog akipozi muda mfupi kabla ya kukabidhiwa cheti chake cha Diploma ya Uwandishi wa habari katika chuo cha uandishi wa habari Zanzibar ZJMMC, mwaka 2011.

Wajumbe wa Kamati Tendaji TASAF Pemba wakipozi kwenye picha ya pamoja huko Chuo cha Amali Vitongoji mara baada ya kumaliza warsha ya kuwajenge uwezo kwenye TASAF awamu ya tatu, ambapo kutoka kushoto ni DC wa Mkoani Jabu Khamis Mbwana, Dc wa Chake chake Mwanajuma Majid Abdalla, Mkurugenzi Mtendaji TASAF Ladis Salsu Mwamanga , RC wa Kusini Pemba Juma Kassim Tindwa akifuatiwa na RC wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi na watendaji wengine wa TASAF makao makuu TASAF (picha na Haji Nassor, Pemba)
Na Haji Nassor, Pemba WAJUMBE wa mpango wa utekelezaji wa TASAF awamu ya tatu kisiwani Pemba, wametakiwa kuwa na ushirikiano wa pamoja, katika kusimamia mpango wa kuzinusuru kaya masikini kwa kuzijengea ufahamu ili zishiriki vyema katika utekelezaji wa miradi. Hayo, yalielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi alipokua akifunga warsha ya siku mbili, iliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha mafunzo ya amali Vitongoji, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Alisema kuwa, lengo kuu la warsha hiyo, ilikuwa ni kukuza uwelewa kwa wadau wote, ambao wanatakiwa kusimamia mpango wa utekelezaji na kuhakikisha kila mwenye vigezo anafaidika katika miradi hiyo. Alisema katika utelezaji wa TASAF kwa amu hii ya tatu mpya, itatekelezwa katika shehia kwa kuzifikia kaya masikini zaidi moja kwa moja, kwa kuzijengea uwezo wa kujiwekea hakiba ambazo zitawasaidia kwa kujipatia maendeleo na kuondokana na umasikini. ‘’Mimi naamini kama sisi viongozi kuanzia ngazi ya shehia ha Mkoa tukijipanga vyema, basi kaya ambazo ni maskini zinaweza kufanikiwa kupubnguza joto walilonalo’’,alisema Mkuu huyo wa Mkoa. Kabla ya ufungaji wa warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania TASAF, Ladis Slaus Mwamanga, alisema, mfuko huo kwa awamu ya tatu, umejipanga vyema ili kuhakikisha kila mlengwa anafikiwa. ‘’TASAF ina kawaida ya kufanikiwa katika awamu zote, hivyo tumeona ni vyema kueleweshana yale mapya, ambayo yanapaswa kujilikana na wote, na kila mapungufu yaweze kuelezwa na kuyafanyia uchambuzi yasiweze kutokea tena'', alisema Mkurugenzi huyo. Mapema, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Juma Kassim Tidwa aliwataka watendaji kushiriki kikamilifu pamoja na kuchangia katika nafasi zao, kuweza kufanikisha malengo ya awamu ya tatu ya TASAF ya kuwaondolea wananchi umaskini. “Natarajia kila mmoja wetu ,atatekeleza vyema majukumu yake kwa wananchi, ambapo wajumbe wa sheha mutakuwa na kazi kubwa ,katika majukumu mbali mbali hivyo naomba muwe makini'', alisisitiza Mkuu wa Mkoa. Kwa upande wake ,Afisa Mdhamin Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Pemba,Amran Masoud Amran, alieleza mpango wa TASAF awamu ya tatu ni kuzisaidia nguvu za wananchi pamoja na kupambana na umasikini kwa kuwapatia wananchi huduma muhimu za msingi. Akitoa mada katika warsha hiyo, muwezeshaji Amadeus Kamagenge, alisema, mpango wa kuziwezesha kaya masikini ,ni kuwaongezea kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu ya wananchi ,ambayo yatafikiwa baada ya utekelezaji. Katika TASAF awamu iliyopita kisiwa cha Pemba, kilibahatika kupata miradi 366 ya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na uvuvi iliyogharimu zaidi ya shilingi 6 bilion na 22 milion. MWISHO.

wajumbe wa Kamati Tendaji wakiwa kwenye picha ya pamoja huko Chake chake Pemba, mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji hao, kwenye awamu ya tatu ya utekelezaji wa TASAF, akiwa na wakuu wa Wilaya na Mikoa ya Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)

Jumatatu, 19 Agosti 2013



VIONGOZI MBALI MBALI WAKISHUHUDIA UTEKETEZAJI W AMISUMENO YA MOTO KISIWANI PEMBA HIVI KARIBUNI, IKIWA NI HATUA YA KUKABILIANA NA UKATAJI MITI OVYO.

Jumapili, 18 Agosti 2013



MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi akiangalia bidhaa za wajasiriamali Pemba, kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Vijana ambapo kwa Zanzibar yalifanyika uwanja wa Madungu Polisi mjini Chake chake Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)

Alhamisi, 15 Agosti 2013

 


MAMBO YA SIKUKUU MKOANI PEMBA MWAKA 2013



Mimili wa blog Haji Nassor, akipoke zawadi baada ya kuwa mwandishi bora kwa Pemba kufuatia shindano lililoitishwa na PPC mwaka 2013

MMILIKI WA BLOG KWENYE SHINDANO AFRIKA KUSINI

Mmiliki wa blog hii Haji Nassor akiwa mbele ya majaji kwenye shindano maalum la Uandishi wa makala za Jinsia, baada mmiliki wa blog hii kushinda katika ngazi ya kitaifa nchini Tanzania mwezi Machi mwaka 2013, na kisha kwenda nchini Afrika kusini kushiriki shindano la kimataifa, ambapo hakufanikiwa kuibuka mshindi mwenzi April mwaka 2013.

Jumanne, 13 Agosti 2013

FIRE WAKIZIMA MOTO MADUNGU CHAKE CHAK 2013D


FIRE WAKIZIMA MOTO MADUNGU

MWAKILISHI WA CAF ALIEMBELE AKIKAGUA UWANJA WA GOMBANI KWA AJILI YA MCHEZO WA TIMU YA JAMHURI NA ST GEORGE YA ETHIOPIA 2013

MSHAURI WA RAIS MAMBO YA SIASA PEMBA SHEHA MOHAMED SHEHA AKIZUNGUMZA NA WANACHAMA ZPDD MJIMBINI

Ongeza kichwa



UONGOZI WA JUMUIA YA UPANDAJI MITI NDONGONI WAMBAA MKOANI PEMBA


DUNI AKIWA PEMBA KUFUNGUA DARAJA LA PUJINI

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR JUMA DUNI HAJI AKIFUNGUA DARAJA LA PUJINI CHAKE CHAKE MWAKA 2013 (PICHA NA HAJI NASSOR)