Jumanne, 12 Novemba 2013
'KAMA MCHEZO VILE' WANAFUNZI wa skuli ya maandalizi ya QAMARIA ya mjini Wete Mkoa wa kaskazini Pemba, wakionyesha mavitu yao kwenye sherehe za siku ya wazazi zilizofanyika ukumbi wa Benjamini Mkapa Wete, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk (picha na Haji Nassor, Pemba)
Jumamosi, 19 Oktoba 2013
'UTULIVU WAHITAJIKA' WANAFUNZI wa skuli ya maandalizi ya Mkoani Pemba, wakiwa kwenye mashindano ya kujaza maji kwenye chupa, ikiwa ni sehemu ya sherehe za siku ya wazazi 'parents day' zilizoenda samba mba na mahafali yao ya kumaliza elimu ya maandalizi ya miaka miwili, sherehe zilifanyika skuli ya Ng'ombeni Mkoani Pemba. (picha na Haji Nassor, Pemba)
Jumamosi, 12 Oktoba 2013
'NATIMIZA AHADI' KULIA ni Meneja wa hoteli ya Manta resort ya Makaangale Micheweni Pemba, Mathew Saus akimkabidhi Mwenyekiti wa wavuvi wilaya ya Micheweni Mkubwa Said Ali, dola 4000, sawa na zaidi ya shilingi 6.4 milioni za Tanzania, ikiwa ni kutimiza ahadi yao kwa wavuvi hao, mara ujenzi wa chumba cha CHINI ya bahari kitakapomalizika (picha na Haji Nassor 12.10.2013)
Jumanne, 1 Oktoba 2013
Alhamisi, 26 Septemba 2013
MKUU wa mkoa wa kusini Pemba Juma Kassim Tindwa, akizungumza na wanajumuia ya JUKAMKUM hawapo pichani kabla ya uzinduzi wa mradi maalum wa kuwafikia vijana 80 wanaotumia dawa za kulevya na waliokatika mazingira hatarishi ya kutumia dawa hizo, hafla hiyo ilifanyika uwanja wa Gombani Chake chake Pemba, kulia ni mjumbe wa JUKAMKUM Fatma Marzouk Kombo na kushoto ni Mussa Mohamed (picha na Haji Nassor, Pemba)
Ijumaa, 20 Septemba 2013
'KAZALIWA 1985- KAFA 2013' Aliekuwa mpiga picha wa kujitegemea kutoka 'the best photo studio' ya mjini Chake chake, Ali Khatib Haji, ambae amefariki dunia tarehe 19/09/2013 majira ya saa 2:40 baada ya kijana huyo kuigonga gari, yeye akiwa na vespa wakati gari hiyo ikikatisha kuelekea Tibirinzi karibu na benki ya watu wa Zanzibar PBZ mjini Chake chake, na kijana huyo akitokea mjini kwenda upande wa Machomane.
'KAZALIWA 1985-2013 KUFA' Aliekuwa mpiga picha wa kujitegemea ''the best photo studio', Ali Khatib Haji wa mji wa Chake chake, akiwa kazini kabla ya kifo chake katika skuli ya Michakaini Chake chake, kijana huyo alifariki kutoka na ajili ya gari baada ya yeye kuigonga gari kwenye eneo la benki ya watu wa Zanzibar PBZ Chake chake, wakati gari ikikaisha kwenda Tibirinzi, tarehe 19/09/2013 saa 2:40 usiku.
Alhamisi, 19 Septemba 2013
Jumamosi, 7 Septemba 2013
''DAR-MPAKA SOUZ'' Mmiliki wa blog hii kushoto mwenye kofia Haji Nassor, akikabaidhiwa TUZO ya uhsindi wa kuwasilisha makala za JINSIA mwezi Machi 2013 huko hoteli ya Blue Parl Ubungo jijini Dar es Salaam, ambapo baadae mwezi April , 2013 sasa safari ikiwa ni SOUZ kwa ajili ya kuiwalikisha Tanzania katika kazi kama hiyo, ingawa hakufanikiwa kushina namba moja.''NIASHINDA? Mmiliki wa blog hii mwenye kofia akifuatilia kwa karibu matokeo ya uwasilishaji wa makala za jinsia Jijini Dar, ambapo badae alishinda na kukabidhiwa tuzo na GENDER LINK
Ijumaa, 6 Septemba 2013
'HAMUPITI HAPA' Mwenye jezi no 6 ni mlinzi wa timu ya Kizimbani Ali Othuman Ali, akisaidiana na mlinzi mwenzake mwenye jezi no 17 Mohamed Juma Mohamed wakiwazuia washambuliaji wa timu Jamuri kwenye mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliochezwa Septemba 6, 2013 uwanja wa Gombani, ambapo Kizimbani ILISHINDA kwa magoli 2-0 (picha na Haji Nassor, Pemba)
'CHUNGA KICHWA CHAKO TU' Mchezo kiumbizi ambao ulikuwa marufu sana katika kijiji cha Pujini Wilaya ya Chake chake, sasa umeonekana kupotea kwa kasi na kuonekana kwenye sherehe za kitaifa pekee (picha na Haji Nassor, Pemba)
'KWANZA NAKATA UTEPE' Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar balozi, Seif alipofika Chambani Wilaya ya Mkoani, kufungua skuli ya kijiji hicho, akishuhudiwa kwa karibu na Naibu Waziri wa Elimu Zanibar Zahara Ali Hamad (picha na Haji Nassor, Pemba)
Jumatano, 4 Septemba 2013
Na Haji Nassor, Pemba
MAHAKAMA ya Mkoa Chake chake, imemuhukumu kifungo cha miaka 60 jela, mshitakiwa Abubakar Mkulu Bakar (28), mkaazi wa Wambaa Mkoani, baada ya kubainika na kosa la kuwabaka watoto wawili mapacha wa kike (13).
Kijana Abuu ametakiwa kutumikia jela kwa muda wa miaka 30 kwa kila mtoto mmoja, baada ya Mahakama hiyo kutosheka na ushahidi uliotolewa na mashahidi sita akiwemo Daktari na watoto wenyewe ambao walibakwa kwa muda wa miaka miwili mfululizo.
Licha ya adhabu hiyo ya kutumikia jela 60, mshtakiwa huyo alitakiwa kulipa fidia ya shilingi laki 200,000 (shilingi laki mbili) kutokana na madhara makubwa aliyowasababishia watoto hao.
Kabla ya mshitakiwa huyo, kupewa adhabu hiyo, upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na mwanasheria wa Serikali Ali Bilali Hassan alisema, kuwa hakuna rikodi ya kosa kama hilo lakini mshtakiwa ana makosa mengine kadhaa Mahakamani hapo.
Bilali alidai kuwa vile vile Mahakama iangalie kosa ambalo mshtakiwa ametiwa nalo hatiani kwamba ni makosa yaliyozoeleka katika jamii hivyo aliomba Mahakama kumpa adhabu kali mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia kama hiyo.
‘’Muheshimiwa Hakimu naiyomba Mahakama yako tukufu kumpa adhabu kali mshtakiwa huyu, ukizingatia jamii inaisema sana Mahakama kutokana na makosa kama haya kwamba hayapatiwi ufumbuzi na kupelekea kuongezeka siku hadi siku ‘’alisema Bilali .
Baada ya hapo, Hakimu Khamis Ramadhan ,alimpa nafasi mshtakiwa, na kuiomba Mahakama imfikirie kwa kumpunguzia adhabu kutokana na kukaa rumande kwa muda mrefu, na kwamba anafamilia inayomtegemea ombi ambalo lilitupwa na Mahkama.
‘’Kama Mahakama imenitia hatiani, Muheshimiwa Hakimu kutokana na tuhuma hizi zidi yangu, naiyomba inionee huruma kwa kunipunguzia idadi ya miaka, ambayo imeniandikia juu ya kosa hili, ambalo lilipangwa juu yangu’’, alidai Abuu.
Awali mshitakiwa Abubakar Mkulu Bakar, alitenda kosa hilo baina ya mwaka 2011 na mwaka 2013 huko Wambaa Mkoani ,Tanga na Mwanza Tanzania baram ambapo ilithibitisha kuwabaka watoto hao kwa pamoja na kuwasababishia maumivu makali katika sehemu zao za siri.
Kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu 125 (1) (2) (e) na kifungu 126 (1) sharia namba 6 ya mwaka 2004, sheria ya Zanzibar iliyopitishwa na baraza la wawakilishi Zanzibar , ambapo pia Mahakama hiyo imetoa haki ya rufaa ndani ya siku 30 kukara rufaa kwa yeyote asieridhika na hukumu hiyo.
Hivi karibuni Mahakama hiyo ya Mkoa Chake chake, ilimuhukumu kifungo cha miaka 15 jela, mshitakiwa Issa Ali Mohamed (28), baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka mtoto wa kike (5) na Ali Mohamed Ali (22) mkaazi wa Kwale Miburani, kifungo cha miaka (30) jela, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike (12).
………………………………………………….. MWISHO ……………………………………………………….
Ijumaa, 30 Agosti 2013
'RURAL REPORTING' Waandishi wa habari waliowengi wamekuwa wakibakia mjini kwa ajili ya kuandika habari za semina, makongamano na kuwaandikia wanasiasa pekee, mmiliki wa blog hii (HAJI NASSOR) kushoto akizungumza na Mjumbe wa Jambo Group iliopo kwanzani Wambaa Mkoani Pemba Mkubwa Haji Bakar, wakati timu ya waandishi wa habari wa Gazeti la Zanzibar leo walipofika kijijini huko (picha na Omar Hassan TSJ)
Jumatano, 28 Agosti 2013
WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo Mgogoni Pemba, akizunguma katika kongamano la vijana, la bara la katiba lililoandaliwa na Jumuia ya Vijana Kaskazini Pemba (NPYO) , kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Said Massoud na kushoto na Mhadhiri wa Chuo kikuu Zanzibar SUZA, Ali Haji Vuia (picha na Haji Nassor, Pemba)
Jumamosi, 24 Agosti 2013
Wajumbe wa Kamati Tendaji TASAF Pemba wakipozi kwenye picha ya pamoja huko Chuo cha Amali Vitongoji mara baada ya kumaliza warsha ya kuwajenge uwezo kwenye TASAF awamu ya tatu, ambapo kutoka kushoto ni DC wa Mkoani Jabu Khamis Mbwana, Dc wa Chake chake Mwanajuma Majid Abdalla, Mkurugenzi Mtendaji TASAF Ladis Salsu Mwamanga , RC wa Kusini Pemba Juma Kassim Tindwa akifuatiwa na RC wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi na watendaji wengine wa TASAF makao makuu TASAF (picha na Haji Nassor, Pemba)
Na Haji Nassor, Pemba WAJUMBE wa mpango wa utekelezaji wa TASAF awamu ya tatu kisiwani Pemba, wametakiwa kuwa na ushirikiano wa pamoja, katika kusimamia mpango wa kuzinusuru kaya masikini kwa kuzijengea ufahamu ili zishiriki vyema katika utekelezaji wa miradi. Hayo, yalielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi alipokua akifunga warsha ya siku mbili, iliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha mafunzo ya amali Vitongoji, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Alisema kuwa, lengo kuu la warsha hiyo, ilikuwa ni kukuza uwelewa kwa wadau wote, ambao wanatakiwa kusimamia mpango wa utekelezaji na kuhakikisha kila mwenye vigezo anafaidika katika miradi hiyo. Alisema katika utelezaji wa TASAF kwa amu hii ya tatu mpya, itatekelezwa katika shehia kwa kuzifikia kaya masikini zaidi moja kwa moja, kwa kuzijengea uwezo wa kujiwekea hakiba ambazo zitawasaidia kwa kujipatia maendeleo na kuondokana na umasikini. ‘’Mimi naamini kama sisi viongozi kuanzia ngazi ya shehia ha Mkoa tukijipanga vyema, basi kaya ambazo ni maskini zinaweza kufanikiwa kupubnguza joto walilonalo’’,alisema Mkuu huyo wa Mkoa. Kabla ya ufungaji wa warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania TASAF, Ladis Slaus Mwamanga, alisema, mfuko huo kwa awamu ya tatu, umejipanga vyema ili kuhakikisha kila mlengwa anafikiwa. ‘’TASAF ina kawaida ya kufanikiwa katika awamu zote, hivyo tumeona ni vyema kueleweshana yale mapya, ambayo yanapaswa kujilikana na wote, na kila mapungufu yaweze kuelezwa na kuyafanyia uchambuzi yasiweze kutokea tena'', alisema Mkurugenzi huyo. Mapema, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Juma Kassim Tidwa aliwataka watendaji kushiriki kikamilifu pamoja na kuchangia katika nafasi zao, kuweza kufanikisha malengo ya awamu ya tatu ya TASAF ya kuwaondolea wananchi umaskini. “Natarajia kila mmoja wetu ,atatekeleza vyema majukumu yake kwa wananchi, ambapo wajumbe wa sheha mutakuwa na kazi kubwa ,katika majukumu mbali mbali hivyo naomba muwe makini'', alisisitiza Mkuu wa Mkoa. Kwa upande wake ,Afisa Mdhamin Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Pemba,Amran Masoud Amran, alieleza mpango wa TASAF awamu ya tatu ni kuzisaidia nguvu za wananchi pamoja na kupambana na umasikini kwa kuwapatia wananchi huduma muhimu za msingi. Akitoa mada katika warsha hiyo, muwezeshaji Amadeus Kamagenge, alisema, mpango wa kuziwezesha kaya masikini ,ni kuwaongezea kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu ya wananchi ,ambayo yatafikiwa baada ya utekelezaji. Katika TASAF awamu iliyopita kisiwa cha Pemba, kilibahatika kupata miradi 366 ya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na uvuvi iliyogharimu zaidi ya shilingi 6 bilion na 22 milion. MWISHO.
wajumbe wa Kamati Tendaji wakiwa kwenye picha ya pamoja huko Chake chake Pemba, mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji hao, kwenye awamu ya tatu ya utekelezaji wa TASAF, akiwa na wakuu wa Wilaya na Mikoa ya Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
