Na Hassan Abu ZJMMC, Pemba
MWANAFUNZI mmoja wa kike (18) anaesoma darasa kumi (Form II), skuli ya binafsi ya Connecting Continent ya Chake chake Pemba , amenusurika kufa, baada kumeza vidonge mchanganiko, baada ya wazazi wake kumkatalia mchumba wake aliempeka kwa wazazi wake.
Tukio hilo lilitokea juzi huko Mkoroshoni Wilaya ya Chake chake Pemba , baada ya wazazi wa mwanafunzi huyo, kumrejesha mchumba wake huyo, ambae alipanga kwa ajili kufunga nae ndoa.
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba Saleh Muhamed Saleh, alisema kuwa mtoto huyo aliamua kuchukua hatua hiyo ya kumeza vidonge mchanganyiko ili kujiua jaribio ambalo hakufanikiwa.
Alisema kuwa, tukio hilo lilitokea Agosti 27 mwaka huu, majira ya saa 2:30 usiku huko Mkoroshoni, ambapo baada ya kumeza vidonge, wazazi wake waliomuona na kufanikiwa kumkimbiza hospitali kwa matibabu.
Kamanda Saleh alimtaja kijana anaedaiwa kusababisha tukio hilo kuwa ni Abdalla Suleiman mkaazi wa Machomane Wilaya ya Chake chake, ambapo mwanafunzi huyo amefanya kosa la jinai kinyume na sheria kifungu namba 215 sheria namba 6 ya mwaka 2004.
Kwa upande wake Daktari dhamana wa Hospitali ya Chake chakeYussuf Hamad amethibitisha kupokea mgonjwa huyo, na amelazwa hospitalini hapo kwa muda wa saa 12 na sasa ameshatolewa na afya yake inaendelea vizuri.
Alisema hawakumfanyia uchunguuzi wa kidamu, kutokana na hali yake haikuwa mabaya sana wakati alipofikishwa hospitali na walimpatia maziwa na dawa nyengine kama huduma ya kwanza.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, amewataka vijana waendelee na masomo yao wasiwe na haraka ya kuingia katika ndoa, kwani sasa ni wakati wakushindana kielimu, na kuwataka wazee nao wawe na msimamo kwa watoto wao.
Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni